Ikram Said Uhamiaji
Michezo Bongo

Ikram Said: Uhamiaji FC Wapo Tayari Kutwaa Ubingwa Zanzibar

Vardo September 18, 2026 3:07 pm

Kiungo mkabaji wa Uhamiaji FC, Ikram Said Ally, ameeleza kuwa kujiunga na miamba hiyo ya Zanzibar ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika taaluma yake, huku akiweka wazi nia yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu huu.

Ikram, ambaye anacheza Ligi Kuu Zanzibar kwa mara ya kwanza msimu huu, anaamini ushirikiano dhabiti ndani ya timu ndio utakaowavusha kileleni.

“Msimu huu naiona Uhamiaji FC ikifika mbali. Naamini tutafanya vizuri na kutwaa ubingwa tukizidisha kushirikiana kati ya wachezaji, bechi la ufundi, na viongozi wetu,” alisema Ikram.


Uhamiaji FC Yaongoza Msimamo Kwa Kasi

Uhamiaji FC imeanza msimu kwa kishindo baada ya kushinda mechi zote nne za kwanza za Ligi Kuu Zanzibar. Wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na:

  • Pointi: 12 (katis ya 12)

  • Mabao ya kufunga: 9

  • Mabao ya kufungwa: 1


Malengo ya Baadaye: Kutoka Zanzibar Mpaka Kimataifa

Pamoja na kuwekeza nguvu kwenye klabu yake ya sasa, Ikram amewasihi wachezaji chipukizi kutokata tamaa na kuendelea kupambana kwani kila kitu kinawezekana.

Akiangazia siku zake zijazo, kiungo huyo aliongeza:

“Malengo yangu makubwa ni kupiga hatua zaidi ya hapa. Ndoto myangu ya siku zote ni kucheza kwenye ligi kubwa zaidi barani Afrika na hata nje ya bara hili.”

Waziri Makonda Asambaratisha Mchakato wa Jezi Mpya Taifa Stars, Auundia Tume Mkataba Safari Mpya Ya Kasino Yaanzishwa Na Chicago Gold 2