Habari za michezo

KAMPENI YA KUJENGA UWANJA…SIMBA WAANIKA WAZI WALICHOKIAMBULIA KWA MASHABIKI…AHMED ALLY AGUNA…

admin June 4, 2022 1:54 pm


Hatimaye Simba imeweka wazi amendeleo ya michango yao juu ya kampeni za ujenzi wa uwanja wao.

Meneja mawasiliano wa Simba, Ahmedi Ally amesema mpaka sasa kupitia kampeni yao ya Tumeanza na tunaweza mashabiki na wanachama wao wamechangia kiasi cha Sh 60 milioni.

Ahmedi amesema fedha hizo bado ziko salama katika malengo yaliyokasudiwa na uongozi wa klabu hiyo.

Aidha Ahmedi amekiri kwamba bado muitikio wa michango hiyo licha ya kuanza kwa kasi bado haitaweza kufikisha malengo yao.

“Michango hii iko salama na tunawashukuru wanachama na mashabiki ambao wameendelea kuchanga,hakuna pesa ambayo itakwenda kutumika kwenye malengo tofauti,amesema Ahmedi.

“Hatuwezi kusema hizi Sh60 milioni tunaweza kujenga uwanja, safari bado ndefu lakini sasa bado tunataka nguvu zaidi ya michango ya Wanasimba,”

KUELEKEA MSIMU UJAO…YANGA WAPANIA KUIBOMOA KAIZER CHIEFS…WAMALIZANA ‘KISIRI SIRI’ NA MASHINE HII YA MAGOLI… MSHAHARA KOCHA MPYA SIMBA NI ZAIDI YA KUFURU…APEWA MASHARTI MAZITO…ADEL ZRANE AKUBALI KURUDI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply