Habari za michezo

PAMOJA NA KUKABIDHIWA TIMU…MATOLA AENDELEA KUWALILIA MABOSI SIMBA…’AKATAA KATAKATA’ MAMBO YA PABLO…

admin June 4, 2022 2:35 am


BAADA ya uongozi wa Simba kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco, Kocha msaidizi Seleman Matola amesema yupo tayari kuiongoza timu hiyo mpaka mwisho wa msimu.

Kocha huyo amesema ujuzi aliochota kutoka kwa makocha wengi aliofanya nao kazi akiwa timu hiyo pamoja na uzoefu wake kwenye ligi ya Tanzania Bara, vinampa kiburi cha kuamini anaweza kufanya kazi hiyo.

“Naushukuru uongozi wa Simba, kwa kunipa nafasi hii ya kuiongoza timu katika nafasi ya kocha mkuu kwa mechi tano zilizobaki kabla msimu kumalizika.Nipo tayari kubeba jukumu hili kutokana na uzoefu niliokuwa nao, cha msingi ni sapoti kutoka kwao na mashabiki pia,” amesema Matola.

Matola amesema hawezi kuzungumzia maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa timu ya kumfuta kazi bosi wake Pablo Franco sababu hilo halimhusu.

Amesema kitu cha msingi kwa sasa ni kuanza mikakati ya kuijenga timu ili msimu ujao irudi kwenye ushindani na kurudisha mataji yote ambayo imeyapoteza msimu huu.

SELELEKA NA BIRIANI LA DStv KWA KUWACHEKI TAIFA STARS WAKIICHINJA NIGER KESHO KWA MTONYO WA BUKU 9,900/= SIKU CHACHE BAADA YA PABLO KUTIMULIWA…SIMBA WAANIKA IDADI YA MAKOCHA WALIOTUMA MAOMBI YA KAZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply