Habar za Usajili Simba

‘BEKI LA KAZI KAZI’ KUTOKA AFRIKA KUSINI LAOMBA USAJILI SIMBA…ALIWAHI KUTAKIWA AKADENGUA….

admin June 12, 2022 3:57 pm


BAADA ya Simba kumnyatia kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio, hatimaye beki kisiki wa Burundi anayekipiga Afrika Kusini, Frederick Nsabiyumva amejipeleka Simba kiaina.

Misimu minne iliyopita, Simba ilikuwa mawindoni kuisaka saini ya beki huyo aliyekuwa Chippa United ya Afrika Kusini, ila ilishindikana kutokana na gharama za kuvunja mkataba na matakwa binafsi kuwa makubwa zaidi ya bajeti ya Simba.

Katikati ya msimu uliopita alimaliza mkataba na Chippa na kugoma kuongeza mwingine kutokana na timu hiyo kushindwa kumuongezea maslahi na kurejea Jomo Cosmos aliyoanzia maisha alivyotua Afrika Kusini kumalizia msimu na sasa yupo huru.

“Misimu iliyopita kulikuwa na mazungumzo na Simba, ila hayakutimia kwa kuwa nilikuwa na mkataba na Chippa. Sasa niko huru na nipo tayari kuzungumza na timu yeyote,” alisema.

“Simba ni timu bora na inashiriki mara kwa mara michuano ya kimataifa hivyo hakuna mchezaji atagoma kuichezea kama wataelewana, ndio maana nimesema kama watahitaji huduma yangu basi ni suala la maongezi tu na tukifikia makubaliano basi nitasaini.” Simba inatafuta beki wa kati mwenye ubora kusaidiana na Henock Inonga na Joash Onyango msimu ujao wakishaachana na Pascal Wawa.

KISA HERSI SAID KUGOMBEA YANGA AKIWA NI MWAJIRIWA WA GSM…WANACHAMA WAIBUKA NA HILI…HOJA 5 ZA MSINGI HIZI HAPA… MWAMBUSI AINGILIA USAJILI YANGA…AWACHANA GSM KUHUSU KUSAJILI MASTAA WA MAANA…”WAVUNJE BENKI”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply