Habari za michezo

LIVERPOOL WAIBWAGA MAN UNITED KWA NUNEZ…APEWA MIAKA 6 YA KUJIVINJARI ANFIELD….

admin June 12, 2022 4:35 pm


DARWIN Nunez yupo mbioni kusaini mkataba wa miaka sita wa kukipiga Liverpool , msimu ujao baada ya kufikia makubalino wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Fabrizio Romano straika huyo anayekipiga Benfica, atatua England kwaajili ya kukamilisha uhamisho wake, baada ya kuondoka kambi ya timu ya taifa ya Uruguay.

Taarifa zimeripoti Liverpool imefikia makubaliano na Benfica kuhusu maslahi binafsi ya straika huyo kabla ya kutambulishwa rasmi Anfield.

Jurgen Klopp alionyesha nia ya kumsajili Nunez kama mbadala wa Saido Mane msimu ujao, aliyetangaza kuondoka dirisha hili la majira ya kiangazi, siku chache baada ya fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya.

Nunez alicheka mara mbili dhidi ya Liverpool ilipomenyana na Benfica kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu uliyopita, na kuzitoa udenda timu zingine kama Manchester United.

Awali straika huyo alihusishwa kuwa yupo mbioni kujiunga na Manchester United, dirisha hili la majira ya kiangazi, hata hivyo katika akaipiga chinia akidai anataka kuichezea timu inayoshiriki Ligi Mabingwa Ulaya.

Nunez amefunga mabao 34 katika mechi zote alizpcheza mashindano yote msimu uliyopita, na katika mashindano ya Ligi Mabingwa Ulaya straika huyo mwenye umri wa miaka 22, amecheka na nyavu mara sita dhidi ya Barcelona, Bayern Munich, Ajax and Liverpool.

MWAMBUSI AINGILIA USAJILI YANGA…AWACHANA GSM KUHUSU KUSAJILI MASTAA WA MAANA…”WAVUNJE BENKI”… KUHUSU ISHU YA BWALYA KUTAKIWA NA AMAZULU FC YA AFRIKA KUSINI…UONGOZI SIMBA WAIBUKA NA HILI JIPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply