Habari za michezo

AHMED ALLY : MTIBWA SUGAR WALIFANYA SIMBA TUKAKOSA UBINGWA WA MSIMU HUU….

admin June 22, 2022 5:50 pm


Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kesho watahakikisha wanawafunga Mtibwa Sugar ili kulipa kisasi walichonacho dhidi yao.

Ahmed ameyasema hayo leo Juni 22, 2022 alipokuwa akielezea matukio ambayo wanatarajia kuyafanya kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa.

“Tunataka kuwafunga kulipa kisasi maana walituharibia harakati zetu za kutafuta ubingwa kwa kutoa sare na sisi, tutawauliza waliipataje ile sare?”alisema Ahmed.

Msemaji huyo alisemba mbali hilo, watautumia mchezo huo kumuaga beki wao Pascal Wawa ambaye mkataba wake umeisha pamoja na kuwaaga mashabiki wa Dar kwani baada ya hapo mechi mbili zilizobaki za Ligi Kuu, wanakwenda kumalizia mkoani.

MERIDIAN BET WAHAMISHIA NGUVU SOKA LA WANAWAKE…MAMBO SASA NI BAMBAM… MAMBO YA KUSHANGAZA ALIYOYAFANYA SADIO MANE KIJIJINI KWAO YAISHTUA DUNIA….ANAHESHIMIKA KULIKO RAIS WAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply