Habari za michezo

UBINGWA WA YANGA KUSHEREKEWA KIULAYA ULAYA AISEE…MAFATAKI YATAKUWEPO KAMA YOTE…

admin June 26, 2022 7:00 am


KLABU ya Yanga imetoa rasmi ratiba yao ya kusherehekea ubingwa kwa kuanza kulipokea Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Yanga jana saa 10:00 jioni ilicheza mchezo wake wa 29 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine, Mbeya na ndipo itakapokabidhiwa rasmi Kombe hilo na baada ya hapo kesho wataanza rasmi kurejea Dar.

Kwa mujibu wa ratiba Yanga itawasili katika uwanja wa Mwl Nyerere saa 5 Asubuhi na msafara utaanza kuondoka uwanja wa ndege saa 5:30 Asubuhi.

Saa 6 mchana viongozi wa Matawi na Wazee wa Jangwani kuwasili makao makuu na saa 8 mchana timu itawasili makao makuu Jangwani.

Saa 8:15 Dua Wazee na Wachezaji na 8:30 Wachezaji watapanda juu ya jengo la makao makuu kuonyesha kombe kisha saa 9 Alasiri chakula cha mchana.

Saa 9:30 Alasiri timu itaondoka Jangwani kwenda Samora  na saa 10 Alasiri timu itawasili Salamander Towe kisha kutakuwa na Burudani mpaka saa 11:00 jioni kutoka kwa wasanii, Juma Nature, Madee, Marioo na Mzee wa Bwax.

Saa 12:30 jioni timu itafungua shampeni na saa 1:00 usiku watafyatua mafataki kwa kuashiria ni mwisho wa sherehe.

RASMI…MBEYA KWANZA YAWA YA KWANZA KUSHUKA LIGI KUU MSIMU HUU…GEITA GOLD WAISOGELEA CAF KININJA… MSUVA AJIPELEKA MWENYEWE YANGA….AFUNGUKA SIMBA WALIVYOMSUMBUA ZAIDI YA MARA 5…GSM WAFANYA KWELI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply