Habari za michezo

KIUNGO WA SIMBA AKATALIWA SINGIDA BIG STARS…WADAI HAYUPO KWENYE MAFAILI…

admin June 28, 2022 12:27 pm


Klabu ya Singida Big Stars, imekanusha tetesi za kuwa kwenye mpango wa kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Kenya Harrison Mwendwa, ambaye aliwasili jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita.

Klabu hiyo ambayo itashiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao (2022/23), imehusishwa na mpango wa kumsajili Mwendwa, baada ya kudaiwa dili lake la kusaini Simba SC limevunjika.

Afisa Mtendaji mkuu wa Singida Big Stars Muhibu Kanu amesema hawana mpango wa kumsajili Mshambuliaji huyo, na wanashangazwa kuona klabu yao imeingizwa kwenye tetesi hizo.

“Hatuna mpango wa kumsajili Mwendwa, kwenye mafaili yangu hakuna kitu kama hicho, unajua wakati huu wa tetesi kila mtu anazungumza lake, lakini niamini mimi kama mtendaji mkuu hakuna mpango wowote wa kumsajili huyu mchezaji.” Amesema Muhibu Kanu.

Kwa sasa inadaiwa kuwa Mwendwa amesharejea nchini kwao Kenya, na anasubiri dili lingine kutoka kwenye klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushindwana na Viongozi wa Simba SC ambao wamedhamiria kufanya maboresho kwenye kikosi chao katika kipindi hiki cha usajili.

WAKATI HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIMNYEMELEA KIMYA KIMYA…MANZOKI AAGANA NA KLABU YAKE UGANDA… RASMI…KUHUSU USAJILI WAKE SIMBA…OKRAH AIBUKA NA KUANIKA KILA KITU…”NI HESHIMA KUBWA KWANGU KUFUATWA ..”.

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply