Habari za michezo

WAKATI HUKU SIMBA NA YANGA ZIKIMNYEMELEA KIMYA KIMYA…MANZOKI AAGANA NA KLABU YAKE UGANDA…

admin June 28, 2022 11:47 am


Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Ceser Manzoki amewaaga rasmi viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu bingwa nchini Uganda Vipers SC.

Manzoki amecheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka miwili na kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2021/22, huku akiibuka kinara wa ufungaji bora.

Mshambiliaji huyo mzaliwa wa DR Congo, ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wa kuaga, huku akiwashukuru wale wote wanaohusika na Vipres SC kwa mazuri waliomfanyia.

“Asante kwa upendo wako, sitasahau.” ameandika Manzoki

Hata hivyo Uongozi wa Vipers ulihitaji kumsainisha mkataba mpya siku chache baada ya Ligi Kuu ya Uganda kufikia kikomo kwa msimu wa 2021/22, lakini alikataa kwa kushinikiza hitaji la Changamoto mpya ya soka lake.

Manzoki aliyetwaa Tuzo tano katika Ligi Kuu ya Uganda msimu wa 2021/22, anahusishwa na mpango wa kujiunga na miamba ya soka nchini, klabu ya Simba SC, inadaiwa tayari ameshafikia makubaliano binafsi na uongozi wa klabu hiyo.

BAADA YA KUFUKUZWA NA AL AHLY….RAIS WA CAF AIBUKA NA HILI KUHUSU PITSO MOSIMANE….ADAI ATAMLIPA MSHAHARA YEYE… KIUNGO WA SIMBA AKATALIWA SINGIDA BIG STARS…WADAI HAYUPO KWENYE MAFAILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply