Michezo Bongo

CHUGA FOUNTAIN GATE NJIA NYEUPE YANGA

Vardo June 23, 2026 8:25 am

WAKATI mashabiki wakizungumza kuhusu kiwango alichoonyesha chipukizi wa Fountain Gate, Juma Abushiri ‘Chuga’ inaelezwa yuko mbioni kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumia Yanga msimu ujao.

Uongozi wa Yanga umechukua uamuzi huo baada ya kuvutiwa na kiwango cha Abushiri alichokionyesha msimu huu pamoja na mechi dhidi yao.

Chuga amekuwa na msimu mzuri wa 2025/2026, alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu baada ya kuisaidia Fountain Gate, kukusanya alama saba katika mechi tatu huku akifunga bao moja na kuchangia kupanda kwa timu kwenye msimamo wa ligi.

Kiwango alichoonyesha dhidi ya Yanga kilizidi kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo kuangalia namna ya kumsajili.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti mabosi wa Yanga walikutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa Fountain Gate pamoja na mchezaji huyo kwa ajili ya kumalizia dili hilo ambalo linaonekana kuingia hatua za mwisho.

Taarifa zinasema mazungumzo tayari yalishaanza kati ya uongozi wa Yanga na Fountain ili kukamilisha dili lake la kuondoka mwishoni mwa msimu huu, hivyo mabosi wa Jangwani wamemwandalia mkataba wa miaka mitatu.

“Makubaliano yanaenda vizuri, kulikuwa na mambo ya mwisho ya kukaa sawa. Mwanzo kulikuwa na wazo la kumsajili kama mchezaji wa timu ya vijana lakini kwa sasa anaelekea kwenda moja kwa moja kikosi cha wakubwa.

“Mara nyingi mechi kubwa zinaamua zaidi kuhusu mchezaji.  Kilichoongeza uzito wa uamuzi huo ni ki-wango ambacho Chuga ameonyesha msimu huu akiwa mmoja wa vijana waliovutia ndani ya Fountain Gate.”

WASIKIE YANGA

Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye hakutaja kutajwa aliliambia Mwanaspoti; “Tulishazungumza na kijana kabla na hakukuwa na shida, kuna mambo mawili yalibaki, kuongea na klabu yake na kumal-izia sehemu ya mazungumzo na yeye mwenyewe mchezaji, tupo eneo salama,” alisema kiongozi huyo.

“Unajua kuhusu kipaji cha huyu kijana sio jambo la kujificha, kila mmoja anaona namna alivyokuwa na uwezo, sasa tunachotaka kufanya ni kumuinua zaidi ili aje kupanda zaidi, tumefanya hivyo kwa wachezaji wengi na sasa wamefanikiwa.

“Tumempa mkataba wa miaka mitatu wenye manufaa mengi kwake, tunataka kumkuza zaidi ndio maana tunamchukua kama mchezaji kijana ambaye hata hivyo atakuwa sehemu ya timu kubwa kwa msimu ujao.

Endapo dili hilo litakamilika, Chuga anatarajiwa kuwa sehemu ya sura mpya ya Yanga msimu ujao huku akipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake moja kwa moja kwenye kikosi cha wakubwa.

MAO AWEKA MALENGO MAKUBWA AZAM FC TPBRC YAGUSA KILIO CHA MABONDIA