Habari za michezo

SINGIDA BIS STARS WAZIDI KUTIKISA USAJILI BONGO…. WAPITA JUMLA JUMLA NA BEKI KISIKI WA YANGA….

admin July 2, 2022 4:57 pm


Klabu ya Singida Big Stars zamani (DTB) imeendelea kushusha vifaa vipya kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata saini ya aliyekuwa beki namba mbili wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’.

Boxer amejiunga na timu hiyo ya ‘Wana alizeti’ kwa mkataba wa miaka miwili kufuatia kushindwa kutamba kwa mabeki Djuma Shaban na Kibwana Shomari hali iliyomfanya kutafuta changamoto sehemu nyingine ili kunusuru kipaji chake.

Wageni hao wa Ligi Kuu Bara huo unakuwa ni usajili wa tatu hadi sasa baada ya kuwatambulisha mshambuliaji, Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza na kiungo Aziz Andambwile aliyesajiliwa kikosi hapo akitokea Mbeya City.

Usajili wa nyota huyo ni muendelezo wa kukisuka upya kikosi hicho kwani baadhi ya wachezaji waliofanikisha timu hiyo kupanda Ligi Kuu wako kwenye hatari ya kutwema hivyo uongozi umeanza maandalizi mapya kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 17.

RASMI….MORRISON AAMUA KULIPELEKA SUALA LAKE KWA RAIS SAMIA…ADAI SIMBA WANAMPONDA LAKINI… PAMOJA NA  JINA LAKE  KUTAJWA TAJWA SANA YANGA….AZIZ ATUA SINGIDA BID STARS,…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply