Habari za michezo

MAMBO YA SAKHO NA SIMBA YAZIDI KUWA BAMBAM…ADHIHIRISHA KUWA YEYE MSIMU HUU NDIYO KILA KITU….

admin July 4, 2022 11:26 am

 


Pape Ousmane Sakho au Mzee wa Kunyunyiza; ni mchezaji wa Simba katika nafasi ya kiungo wa kisasa mwenye uchezaji mzuri wa mpira, ujuzi na haraka ambaye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Sakho, raia wa Senegal amewapiku wakali wenzake wawili, Peter Banda na Kibu Dennis ambao pia walikuwa kwenye kinyangโ€™anyiro hicho.

Sakho amepata jumla ya kura 445 sawa na asilimia 58.71 akifuatiwa na Banda aliyepata kura 234 (30.87%) huku Kibu akipata kura 79 sawa na asilimia 10.42. Katika mwezi Juni, Sakho amecheza mechi tatu kati ya tano sawa na dakika 221 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana mawili.

Sakho amekabidhiwa tuzo na fedha taslimu sh. Mil 2 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Sakho kunyakua tuzo hiyo, aliwahi kuipata mapema Januari mwaka huu.

WAKATI LIGI ZIKIWA ZIMESIMAMA DUNIANI KOTE…DStv BADO WAKO NA WEWE…NA SAFARI HII NI KWA AFCON YA WANAWAKE … BAADA YA KUMALIZA MKATABA NA KMC….SHIKALO AVUNJA UKIMYA….ADAI MALENGO YAKE YAMETIMIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply