Habari za michezo

KISA KOMBE LA SHIRIKISHO KUHARIBIKA MIKONONI MWAO…YANGA WATOA TAMKO …BUMBULI ADAI LINA SKRUU…

admin July 6, 2022 9:44 am


Ofisa Habari wa Yanga SC, Hassan Bumbuli ameeleza kuwa skruu ya Kombe la ASFC ilikuwa imelegea kutokana na kushikwa na watu wengi.

Bumbuli ameeleza hayo leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kusambaa kwa video ikionyesha Kombe la Azam Sports Federation kama limevunjika.

“Kilichotokea ambacho kinasambaa na watu wanakisambaza mtandaoni lile Kombe huwa kuna wakati linasafishwa huwezi ukaliweka likakaa vile.

“Kuna wakati limepigwa vumbi linatakiwa lisafishwe kwahiyo wanaweka skruu kwa ajili ya kulifungua hiki mnakisafisha peke yake, kile pake yake mnakirudishia.

“Kwasababu sisi ni wengi huyu kalishika yule kalishika skruu ikawa imelegea. Lakini kombe lipo liko imara zuri,” amesema Bumbuli.

KISA KUIFUNGA YANGA GOLI TATU MWENYEWE…AZAM FC WAZIDI KUPAGAWA NA SOPU….MSEMAJI WAO KAIBUKA NA HILI JIPYA… BAADA YA KUMALIZANA NA ISHU YA MANARA …JEMEDARI SAIDI AMVAA INJINI HERSI…AMPONDA KWA KUOMBA KURA NA KOMBE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply