Habari za michezo

RASMI…MUGALU ARUDI KWAO DR CONGO….TIMU KUBWA NNE AFRIKA ZAMNYANTIA…SIMBA WABAKI KIMYA….

admin July 7, 2022 4:04 pm


Mshambuliaji wa Simba, Chriss Mugalu ameondoka nchini na kwenda kwao DR Congo huku akiwa hafahamu hatma yake ya msimu ujao kutokana na mvutano unaoendelea ndani kwa mabosi wake.

Hata hivyo, inajulikana kwamba Mugalu ana ofa za timu nne mkononi anazunguka nazo ambazo mabosi wake ndiyo wataamua kwani bado ana mkataba na Simba.

Miongoni mwa timu zilizoonyesha nia hiyo ni Zesco United, Nkana Red Devils, Power Dynamos zote za Ligi Kuu Zambia pamoja na FC Saint-Eloi Lupopo inayoshiriki Ligi Kuu DR Congo.

Mugalu alipojiunga Simba Agosti 2020, akitokea Dynamos alisaini mkataba wa miaka miwili ambao ndani yake ulikuwa na nyongeza ya mwaka mmoja na kuwa mitatu ambao sasa umebaki mmoja.

Mugalu ana mkataba Simba lakini kuna mvutano unaoendelea kwani baadhi ya viongozi wanataka waachane naye kutokana na kiwango chake msimu uliopita kuwa chini huku wengine wakitaka apewe muda zaidi.

Mugalu hakufanya vizuri msimu huu kutokana na kuwa na majeraha ambapo amemaliza ligi bila kufunga bao hata moja katika mechi alizopata nafasi ya kucheza tofauti na msimu uliopita akimaliza na mabao 15.

Alipotafutwa Mugalu alisema ameenda kwao kwa ajili ya mapumziko ila bado ana mkataba na Simba unaomalizika msimu ujao huku akidai kama kuna ishu nyingine basi si rasmi.

TECNO YAZINDUA SIMU MPYA  KALII YA CAMON 19… YENYE KUPIGA PICHA KALI HASA USIKU…. IKIWA IMEPITA MWEZI TOKA AJIUNGE NA SIMBA….MOSES PHIRI AIBUKA NA HILI KUBWA KUHUSU CHAMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply