Habari za michezo

BAADA YA FIFA KUMPA HAKI YAKE DHIDI YA WAARABU…MSUVA AFUNGUKA HAYA KUHUSU KUJIUNGA NA YANGA…

admin July 12, 2022 3:09 pm


Aliyekuwa mchezaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Simon Happygod Msuva amesema anafahamu kuwa mashabiki wa Yanga wanataka arejee katika Klabu hiyo lakini yeye kwa sasa anatazama kucheza nje ya Tanzania kwanza.

Msuva jana ilitoka taarifa ya FIFA kuwa ameshinda kesi yake dhidi ya Wydad na wanatakiwa wamlipe pesa anazowadai kiasi cha Tsh bilioni 1.6.

“Mimi sikuondoka vibaya Yanga SC, najua wengi wanatamani nirudi Yanga SC. Sitaki kuwakatisha tamaa ipo siku nitarudi Yanga SC. Lakini kwa sasa bado natamani kucheza nje,” amesema Msuva.

Sasa Msuva yuko huru kujiunga na timu yoyote huku Yanga ikitajwa kumnyemelea staa wao aliyemaliza msimu wake wa mwisho Jangwani akiwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 14.

STAA MPYA WA YANGA ALIYECHEZA NEWCASTLE AFUNGUKA SABABU YA KUJA TZ…ADAI WAKO WENGI WATAKUJA… MO AONGEZA NGUVU USAJILI SIMBA….STRAIKA MNIGERIA KUFUNGA USAJILI…MISHAHARA YA MASTAA WAPYA YANGA TISHIO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply