Azam FC

KUELEKEA MSIMU UJAO…AZAM WATAKA KUFANANA NA SIMBA KILA KITU…NAO WAPANGA KUIFUATA AL AHLY…

admin July 12, 2022 8:40 am


Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza rasmi kuweka kambi nchini Misri katika mji wa Al Ghouna kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Azam inatarajia kuondoka nchini Julai 18 na kurejea nchini Agosti 12.

Akizungumza msemaji wa klabu hiyo Thabit Zakaria ‘Zaka’ amesema sababu kubwa ya kuchagua kwenda nchini Misri ni kwa sababu hawajahi kuweka kambi nchini humo.

Zaka amesema wakiwa Misri watacheza michezo kadhaa kisha watarudi nchini kuendelea na ratiba zingine kwa ajili ya Ligi Kuu na Mashindano mengine.

“Wachezaji wataanza kuingia kambini kuanzia tarehe 15 mwezi huu halafu kutakuwa na vipimo na mambo mengine, Julai 18 tutaanza mazoezi hapa hapa halafu ndio tutaondoka,” amesema Zaka na kuongeza;

“Tungeweza kwenda sehemu nyingine lakini pale kuna utulivu, tulishaenda Afrika Mashariki, kusini na kati na safari hii tumeona twende huku.”

KUELEKEA MSIMU UJAO…MTIBWA SUGAR WASHTUKA JAMBO…WAANZA KUTEMBEA NA ‘BITI’ LA SIMBA NA YANGA… BAADA YA KUTUA AZAM FC…..SOPU AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA NAMNA ISHU NZIMA ILIVYOKUWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply