Azam FC

AZAM FC WAJIBU MAPIGO SIMBA….NAO WASHUSHA KIFAA CHA MAANA KUTOKA GHANA…HUYO OKRAH CHA MTOTO…

admin July 15, 2022 8:55 am


Klabu ya Azam ni kama safari hii wameamua kuiiga Simba kwa kila kitu, kwanza wakati Simba wakisema wanaenda Misri kwa kambi, nao haikuchukua muda wakatangaza kwenda Misri, pili baada ya Simba kumsajili mchezaji kutoka Ghana, nao wameimeingia mkataba wa miaka miwili na kiungo mshambuliaji, Mghana James Akaminko, akitokea Great Olympic.

Akaminko, 26, ambaye ni mmoja wa viungo wabunifu, aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Tunisia katika timu ya US Tataouine, pia amepita kwa vigogo wa Ghana, Ashanti Gold na Medeama.

Mbali na kucheza eneo la ushambuliaji, pia anao uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji, na anakuja kuongeza nguvu katika eneo la kiungo kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo, hii huenda inatokea na sio kwamba kunakuigana, kwani kipindi hiki klabu za soka duniani kote zipo kwenye hekaheka ya usajili na kujiimarisha kwa msimu ujao.

BAADA YA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA….BOSI SportPesa AIBUKA NA HAYA….ADAI WALIFURAHI KUACHANA NAO… GUNDU LA KUFUKUZWA LAZIDI KUMTAFUNA MESUT OZIL…ATUPIWA VIRAGO NA FENERBAHNCE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply