Habari za michezo

KISA MORRISON KURUDI NYUMBANI…’KIPENSELI’ ATUPIWA VIRAGO YANGA…KASEKE NAYE AONYESHWA MLANGO WA KWENDA…

admin July 15, 2022 8:44 am


Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na kiungo mshambuliaji, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ baada ya kandarasi yake kumalizika.

Balama alijiunga na Yanga Juni 22,  2019 akitokea Alliance ya Mwanza na kuonyesha kiwango kizuri ingawa majeraha ya mara kwa mara yalimfanya kushindwa kuwika hali iliyopelekea mabosi wa timu hiyo kuachana naye baada ya kudumu kwa miaka mitatu.

Licha ya majeraha yake ila ujio wa nyota wengine wapya kwenye kikosi hicho wakiwemo, Bernard Morrison, Gael Bigirimana na Aziz KI ungezidi kutishia nafasi yake ya kucheza.

Nyota huyo anakuwa wa pili kuachwa na Yanga msimu huu baada ya hapo awali kutangaza kuachana na Deus Kaseke ambao wote mikataba yao imeisha.

MAYELE APANGA KUITUMIA SIMBA SC KUJITAMBULISHA …”SITATETEMA TENA”…. BAADA YA SIMBA KUPATA MDHAMINI MPYA….BOSI SportPesa AIBUKA NA HAYA….ADAI WALIFURAHI KUACHANA NAO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply