Habari za michezo

HABIB KYOMBO ARITHISHWA ‘MIZIGO’ YA MORRISON SIMBA…AANZA NAYO KAZI RASMI KWENYE MECHI NA WAARABU…

admin July 21, 2022 4:06 pm


Straika mpya wa Simba, Habib Kyombo amekabidhiwa majukumu mapya baada ya kupewa jezi namba tatu aliyokuwa anavaa staa wa zamani wa timu hiyo, Bernard Morrison.

Morrison ambaye amejiunga na Yanga kwa ajili ya msimu ujao, akiwa na jezi hiyo kwenye kikosi cha Simba, ameonyesha ubora upande wa mashindano ya kimataifa baada ya kupiga pasi nne za mabao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na kuifanya Simba kuingia hatua ya robo fainali msimu uliopita.

Kyombo kwa mara ya kwanza alivaa jezi hiyo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ismaily nchini Mirsi na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kyombo ana kazi ya ziada kuonyesha thamani yake kwani sio tu kurithi jezi ya Morrison bali hata upande wake mwenyewe usajili wake mashabiki na wapenzi wa soka waliupigia kelele huku ukigubikwa na sintofahamu baada ya kusaini awali Singida Big Stars.

Mshambuliaji huyu msimu uliopita akiwa na Mbeya Kwanza alifunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao, lakini hazikutosha kuibakisha timu hiyo kwenye ligi.

Simba imeweka kambi Misri ikijiandaa na msimu mpya na itacheza mechi kadhaa za kirafiki ikiwa ni sehemu ya kuweka miili sawa kabla ya msimu wa mashindano mbalimbali haujaanza.

BAADA YA KUSIKIA MANENO YA KUKATALIWA NA MASHABIKI….MUGALU AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA YALIYOMSIBU… BAADA YA KUPATA TIMU MPYA SAUDI ARABIA….MSUVA AWAACHIA WATANZANIA UJUMBE HUU…”NIPO TAYARI KWA MAPAMBANO”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply