Habari za michezo

KAMBI YA MISRI YAMFANYA MATOLA KUFUNGUKA HAYA MENGINE KUHUSU UONGOZI WA SIMBA…

admin July 28, 2022 8:46 am


Kocha Msaidizi Seleman Matola, ameupongeza uongozi pamoja na Kamati ya Usajili kwa kufanya usajili ambao umeziba mapungufu yote yaliyokuwepo msimu uliopita.

Matola amesema kwa sasa kila namba kikosini ina wachezaji bora zaidi ya mmoja hivyo imeongeza ushindani mkubwa mazoezini kila mmoja anajitahidi kulishawishi benchi la ufundi.

Matola pia ameupongeza uongozi kwa kumleta Kocha Zoran Maki ambaye falsafa zake zinaendana na timu hivyo imekuwa rahisi wachezaji kuelewa anachofundisha.

β€œLeo ni siku ya 11 tangu tulivyoanza kambi yetu hapa Misri, jambo zuri ni kwamba imekuwa rahisi kwa wachezaji kuelewa mafunzo ya kocha na hii inatoka falsafa yake inaendana na timu.

β€œNiupongeze uongozi kwa kufanya usajili mzuri pamoja na kumleta kocha Zoran. Mimi niwahakikishie msimu ujao tutakuwa na timu imara ambayo kila Mwanasimba ataifurahia,” amesema Matola.

BAADA YA KUUMALIZA MSIMU ULIOPITA AKIWA HOI …PRINCE DUDE KAJITIKISA NA KUFUNGUKA HAYA KUHUSU AZAM FC… RASMI….SIMBA KUWAPITISHIA FAGIO LA CHUMA MUGALU NA KAGERE…ISHU YA MANZOKI SAWA NA PUA NA MDOMO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply