Habari za michezo

BAADA YA KUIFUNGISHA MDOMO YANGA…MASTAA VIPERS WAIBUKA NA KUWAPONDA KINA AZIZ KI…

admin August 8, 2022 11:20 am


Wachezaji wa Timu ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers Sc wameaponda mabeki wa Yanga wakisema kuwa hawana kasi ndio maana ilikuwa rahisi kwao kupenya kirahisi ngome ya Yanga na kuwatungua kirahisi.

Wachezaji hao wamesema hayo wakihojiwa na wanahabari mara baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Vipers na Yanga kukamilika katika Dimba la Mkapa na Vipers kuibuka na ushindi wa bao 2-0 juzi Jumamosi, Agosti 6, 2022.

“Yanga watengeneze timu kwanza, hata sisi tulikuwa hivyo hivyo lakini tukatengeneza timu yetu polepole mpaka hapa ilipofikia leo.

“Tatizo tuliloiona kwa Yanga ni mabeki wao hawana kasi, sisi washambuliaji wetu wana kasi ndio maana walikuwa wanawaacha mabeki wa Yanga. Sisi mechi ya leo (juzi) imetuongezea nguvu na maandalizi yetu yalikuwa mazuri,” wamesema wachezaji hao.

Kwa upande wake straika aliyekuwa akihusishwa kutua Simba, Cesar Manzoki amesema; “Japo sijacheza lakini tumeshinda bao 2-0, mechi ilikuwa nzuri sana, tunaiheshimu Yanga ni timu nzuri.”

Mabao ya Vipers yalifungwa na Milton Karisa dakika ya kwanza ya mchezo huku bao la pili likifungwa na Anukani Bright dakika ya 64.

KUELEKEA MKUTANO MKUU WA CAF TANZANIA….RAIS SAMIA KUZINDUA ‘SHOW’….RAIS KENYATTA KUIBEBA SUPER LEAGUE… #SIMBADAY: MKUDE AWEKA REKODI YA KIBABE SIMBA…MAKOCHA 14 WAPITA NAYE JUU KWA JUU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply