Habari za michezo
KIGWANGALA : JEZI NZURI ILA MJADALA WA BILIONI 20 ZA MO DEWJI UKO PALE PALE….NIMEAMUA KUNYAMA NISIHARIBU LADHA…
Mbunge wa Nzega Vijijini na Shabiki wa Simba, Hamis Kigwangalla amesema suala la mjadala wa Bilioni 20 zilizoahidiwa na Mwekezaji Mo Dewji kwa Simba SC liko palepale lakini hiyo haimzuii kupongeza kuwa jezi mpya za Simba zilizooneshwa leo ni nzuri.
“Mjadala wa 20B uko pale pale lakini siwezi kupinga kila kitu hata wanavyopatia, mimi siyo ‘hater’ naheshimu na kushukuru juhudi na kazi nzuri, sinaga unafiki wa kusifia upuuzi…jezi hizi ni nzuri, kuna maeneo sikubaliani nao lakini nimeamua kunyamaza nisiharibu ladha”
Kwenye mfululizo wa tweets zake Kigwangalla aliandika “Jezi yetu kali sana kwa Watu wenye body zao unyama ni mwingi sana,” amesema Kigwangallah.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.