Habari za michezo

MRITHI WA SENZO YANGA AFICHUA DILI LA MANZOKI NA SIMBA….AFUNGUKA ATAKAVYOTIKISA LIGI KUU NA KUWA MSAADA…

admin August 8, 2022 3:13 am


MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Yanga Simon Patrick amesema usajili wa Cesar Lobi Manzoki ndani ya Simba ni usajili mzuri na wa kiwango cha juu ambapo amemwagia sifa mshambuliaji huyo wa Vipers kuwa atawasaidia watani wao klabu ya Simba.

“Manzoki ni mchezaji mzuri sana na ni kitu ambacho naweza nikawapongeza watani zetu wamepata mchezaji mzuri na tuna Imani atawasaidia namtakia kila lakheri ni mchezaji mzuri tunampenda sana na tunamsapoti akiwa hapa Tanzania.” amesema Simon Patrick

Aidha CEO ameongelea kuhusu tukio la kilele cha wiki ya wananchi ambapo amebainisha kuwa waliuza tiketi 54000 .

Yanga ilicheza dhidi ya Vipers ya nchini Uganda katika mchezo wa kirafiki kuazimisha wiki ya wananchi, mchezo ambao ulichezwa majira ya saa 1 kamili usku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

NGOJA TUNUWAONESHE…SIMBA YATAMBA MAPEMA ..LEO KUNA SAPRAIZI NYINGINE ‘KULALEKI’….PITSO ATOA NENO… RONALDO AKUCHA USO KAMA ‘MWANAMKE’ MAN UTD WAKIPOKEA KICHAPO ….WAANZA LIGI NA GUNDU, BALAA NA MIKOSI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply