Habari za michezo

IMETIKI…..BAADA YA KUSUSWA NA TIMU ZA BONGO….KABWILI APATA TIMU RWANDA….MCHONGO MZIMA KAZE ANAUJUA…

admin August 18, 2022 9:44 am


Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili amejiunga rasmi na Klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kabwili ambaye alimaliza mkataba wake na Yanga, amekamilisha dili hilo huku ikielezwa kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze akihusika.

Timu hiyo ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya nne inahitaji kurejesha heshima kwenye soka la nchi hiyo huku ikiamini usajili wa kipa huyo utawasaidia kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Kabwili aliyewika na Serengeti Boys iliyoshiriki AFCON ya vijana 2017 nchini Gabon alipendekezwa na kocha wa makipa wa timu hiyo Mrundi, Vladimir Niyonkuru aliyewahi kufanya kazi nae ndani ya Yanga miaka kadhaa nyuma.

Kipa huyo alianzia Akademi ya Azam kisha kuhamia Yanga alipokaa kwa miaka mitano kabla ya kumaliza mkataba wake msimu huu.

MAPYA YAIBUKA ISHU YA MANZOKI KUTUA SIMBA…AZIZ KI APEWA UFALME YANGA…MAYELE AMJAZA UPEPO NABI… HUYU HAPA DEJAN GEORGIJEVIC…MTAMBO WA MABAO SIMBA KUTOKA ULAYA….AAPA KULIPA KISASI CHA KUZOMEWA NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply