Habar za Usajili Simba

ZILE TETESI ZA MUDATHIRI YAHYA KUTUA SIMBA ZIKO HIVI….MAMBO YANAENDA KIMYA KIMYA AISEEE….

admin August 19, 2022 3:54 pm


Kiungo wa zamani, Azam FC na Singida United, Mudathir Yahya ameingia kwenye rada za Simba ambao wapo sokoni kutafuta kiungo mpya wa ukabaji kutokana na kutolizishwa na ubora waliokuwepo sasa.

Inaelezwa mabosi wa Simba walifanya mawasiliano yenye usiri mkubwa na Mudathir ambaye kwa sasa ni mchezaji huru ila hakutoa majibu yoyote kama yupo tayari kujiunga na timu hiyo.

Mabosi hao wa Simba inaelezwa wanapambana na kutafuta kiungo mpya wa ukabaji huku, Afeez Nosiru kutokea Kwara United ya Nigeria ndio anapewa nafasi kubwa kama chaguo la kwanza kwenye usajili wa nafasi hiyo.

Mudathir kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Azam kuna nyakati aliwahi kueleza amepanga kupumzika kucheza mpira hadi dirisha dogo la usajili ndio atafanya maamuzi timu mpya ambayo atakwenda kuichezea.

KIULAINIII KABISA …FAHAMU JINSI YA KUSHINDA JACKPOTI YA MERIDIANBET NA UTUSUE KIMAISHA… KISA UWEPO WA SAKHO NA BANDA…WAPINZANI WA SIMBA CAF WAANZA KUPAGWA….WAAMUA KUJA NA MBINU ZA KIJASUSI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply