Habari za michezo

BAADA YA KUSIKIA STORI ZA KUTAKA KUTEMWA….KAMBOLE KAPONA NA KUANZA MAZOEZI FASTA…DIARA KUKOSEKANA MECHI YA LEO…

admin August 20, 2022 11:35 am


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Lazarious Kambole ameanza rasmi mazoezi kwenye kikosi hicho tayari kwa ajili ya kujiweka fiti kwenye michezo inayowakabili klabu hiyo msimu huu.

Kambole ambaye ni raia wa Zambia alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha hili kubwa la usajili akitokea Kaizer Chiefs baada ya mkataba wake kumalizika.

Tangu kuanza kwa msimu huu ambapo Yanga tayari imecheza mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania nyota huyo hajacheza kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Akizungumzia hali ya kikosi kuelekea mchezo huo dhidi ya Coastal Union, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kuwa kikosi kimekamilisha maandalizi.

“Kikosi kimekamilisha maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union na tunaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo.

“Kambole ameanza kufanya mazoezi leo (jana) asubuhi na timu lakini hatujamjumuisha kwenye mipango yetu ya mchezo dhidi ya Coast Union.

“Tofauti na Yacouba Songne ambaye ana majeraha ya muda mrefu wachezaji ambao watakosekana kwenye mchezo dhidi ya Wagosi wa Kaya ni Djigui Diarra na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.”

ULE MPAPATUKO WA LIGI KUU YA NBC..KUENDELEA TENA LEO…WAKUBWA WOTE ‘MACHO KODO’ KWENYE VIWANJA WIWILI…. HUYU HAPA STAA WA YANGA ANAYETAKIWA NA MARSEILLE YA UFARANSA…MWINYI ZAHERA TOA LA MOYONI KUHUSU DILI HILO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply