Habari za michezo

FT: COASTAL UNION 0-2 YANGA SC…MAYELE KAMA KAWA AENDELEZA ALIPOISHIA…MORRISON AANZA KUWAKERAAAH….

admin August 20, 2022 8:30 pm


Kama walivyomaliza Ligi ndivyo walivyoanza msimu huu baada ya hii leo Klabu ya Yanga kuitandika Coastal Union magoli 2-0 ugenini mchezo wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri abeid, umewashuhudia Yanga wakianza na mabadiliko katika kikosi chao kwa kutokuwa na golikipa Djigui Diarra, Beki Dickson Job huku Fiston Mayele akianzia benchi.

Iliwachukua Yanga dakika 4 tu kujiandikia bao la uongozi kupitia kwa Bernard Morisson.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Yanga walikua kifua mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi huku wakicheza soka safi na dakika ya 67 Fiston Mayele alieingia akitokea benchi akawahakikishia Wananchi alama tatu kwa bao lake la kichwa.

Mpaka sasa Fiston Mayele amecheza michezo miwili na kufunga magoli mawili.

Kwa ushindi huo Yanga wanakwenda kileleni katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 6.

FT: SIMBA 2-0  KAGERA SUGAR …..BAADA YA KUITWAAA SANAAAH..’MZUNGU’ NAYE KAITIKA KIULAYA ULAYA…PHIRI KAMA KAWA…. WAKATI YANGA WAKIWEKA REKODI MPYA LIGI KUU…DEJAN AANZA KUTUPIA KWA NGUVU…AKPAN AFUNGUKA MAZITO SIMBA SC..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply