Habari za michezo

ISHU YA AKPAN NA KAPAMA KUKATALIWA NA MAKI SIMBA….GEOFF LEO ‘AWANYEA’ VIONGOZI KWA UBINAFSI…

admin August 20, 2022 2:40 am


Siku chache tangu wajiunge na Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club wachezaji Victor Akpan na Nassoro Kapama wametajwa kutokuwa katika mipango ya kocha Zoran Maki.

Mjadala wa wawili hao umezidi kuwa mkubwa midomoni mwa wapenda soka wakishangaa inakuwaje kuachwa pasipo kupewa nafasi huku Ligi ikiwa ndio kwanza imeanza.

Sasa mchambuzi wa soka kutoka kituo cha EFM/TVE Geoff lea nae amezungumzia sakata la wachezaji hao.

“Victor Akpan na Kapama hawakuwa na kitu spesho katika ligi ya msimu uliopita, ukimuoma mchezaji anacheza nafasi nyingi ujue hana utaalam kwenye nafasi moja, Simba ilikuwa kubwa kwa akpan bora angeenda KMC kwa sababu alichokionesha akiwa na Coastal Union hakikuwa kitu kikubwa kiasi hicho. Viongozi ndio waliowasajiliwa hawa”

Victor Akpan alisajiliwa na Simba akitokea Coastal Union, huku Nassoro Kapama akitokea Kagera Sugar.

Ujio wa wachezaji hao ndani ya Simba haukuwa wa kufurahisha mashabiki tangu awali na sasa kuondoka kwao ni kama kuthibitisha yale waliyokuwa wakisema mashabiki.

FILAMU YA MANZOKI…SIMBA NA YANGA MACHO ‘KODO’…ZORAN AWAKATAA MASTAA 5…NABI AMTIA ‘PINGU’ AZIZ KI…. SIKU CHACHE BAADA YA KUJITABIRIA KIFO…..HALI YA AFYA YA MIKE TYSON YAANZA KUZOROTA…AANZA KUTUMIA ‘WHEELCHAIR’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply