Burudani

SIKU CHACHE BAADA YA KUJITABIRIA KIFO…..HALI YA AFYA YA MIKE TYSON YAANZA KUZOROTA…AANZA KUTUMIA ‘WHEELCHAIR’….

admin August 20, 2022 2:45 am


Bondia Mkongwe Mike Tyson (56) ameonekana akiwa mdhoofu kwenye kiti cha magurudumu (wheelchair) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Miami.

Tyson ambaye ni mmoja wa mabondia waliofanikiwa sana kwenye mchezo huo duniani alistaafu mwaka 2005, hata hivyo amekuwa akirudi ulingoni mara kadhaa katika mfumo wa maonyesho.

Taarifa zinasema kuwa Tyson anasumbuliwa na matatizo ya mgongo yanayotokana na jeraha.

Hivi karibuni akiwa jijini New York bondia huyo mstaafu alihitaji kutumia fimbo ili kuweza kupata balansi ya kutembea.

Picha hizi zimezua wasiwasi kati ya mashabiki zake baada ya hivi karibuni Tyson kuutabiri mwisho wake kupitia kipindi cha HotBoxin ambapo alisema

”Wote tutakufa siku moja bila shaka. Nikijiangalia kwenye kioo, nayaona mabadiliko usoni mwangu, hii inaamaanisha tarehe ya kumalizika kwangu iko karibu,” alisema Tyson hivi karibuni.

ISHU YA AKPAN NA KAPAMA KUKATALIWA NA MAKI SIMBA….GEOFF LEO ‘AWANYEA’ VIONGOZI KWA UBINAFSI… KUELEKEA FAINAL KOMBE LA DUNIA…MASHABIKI WAZIDI KUMIMINIKA QATAR…MAUZO YA TIKETI YAVUNJA REKODI YA DUNIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply