Simon Dladla Yanga SC
Yanga SC

Dladla Afunguka Mazito Yanga Walipokutana na Mashujaa FC: “Bao la Mapema Lilituvuruga”

Vardo October 28, 2026 12:54 pm

KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga SC, Simon Dladla, amefunguka kuwa bao la mapema walilofungwa na Mashujaa FC liliweka kikosi chake kwenye wakati mgumu, baada ya wapinzani wao kubadilisha mbinu ghafla na kujilinda kwa idadi kubwa ya wachezaji.

Dladla ameeleza kuwa bao hilo liliilazimisha Yanga kucheza kwa presha kubwa ya kusaka bao la kusawazisha, hali iliyowafanya wachezaji wake kushindwa kutumia vizuri nafasi za wazi walizozitengeneza langoni mwa Mashujaa.

“Mechi ilikuwa ngumu sana baada ya kuruhusu bao lile la mapema. Tulilazimika kuongeza presha ili kusawazisha, lakini wapinzani wetu walibadilisha mfumo na kuanza kujilinda kwa wingi. Hilo lilitupa wakati mgumu sana kuwavunja na kupata mianya ya wazi,” amesema Dladla.

Kocha huyo aliongeza kuwa presha ya kutafuta matokeo kwa haraka iliathiri umaliziaji wa safu yake ya ushambuliaji, kwani wachezaji walipoteza utulivu katika eneo la mwisho. Alitolea mfano nafasi ya wazi aliyosaulika kuitumia mshambuliaji Jalaal alipobaki ana kwa ana na kipa wa Mashujaa FC.

Mabadiliko ya Kipindi cha Pili na Majeraha

Akimulika zaidi mwenendo wa mchezo, Dladla alisema aliridhishwa na kiwango cha timu yake katika kipindi cha kwanza licha ya changamoto ya umaliziaji, lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili kutokana na majeraha yaliyomlazimisha kufanya mabadiliko kadhaa.

“Kipindi cha kwanza niliridhishwa na namna wachezaji walivyoitikia baada ya kufungwa, isipokuwa tu changamoto ya kutotumia nafasi. Lakini kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwa sababu tulilazimika kufanya mabadiliko mengi yasiyotarajiwa kutokana na majeraha ya wachezaji,” aliongeza.

Licha ya changamoto hizo zote, Dladla alipongeza jitihada na ubora wa wachezaji wake waliopambana na kuibuka na ushindi, ingawa amesisitiza kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kuimarisha eneo la umaliziaji kabla ya michezo ijayo.

Kauli ya Fadlu Davids Yanga SC Yaibua Mzuka Mpya Jangwani Liverpool, Chelsea; Mmoja Kutoka Leo Carabao Cup