Ally Kamwe Yanga SC
Yanga SC

Ally Kamwe Afunguka Changamoto za Ndani Yanga SC Dhidi ya Mashujaa FC

Vardo October 28, 2026 12:35 pm

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, amekiri kuwa timu hiyo haikuonyesha kiwango chake bora cha ushindani katika mchezo wao dhidi ya Mashujaa FC licha ya kuondoka na ushindi wa pointi tatu muhimu.

Kamwe amefichua kuwa kulikuwa na changamoto za ndani ya klabu ambazo viongozi walikuwa wakizishughulikia nyuma ya pazia, jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa wachezaji kushindwa kucheza katika kiwango chao cha kawaida.

“Tumeshinda, lakini hatukuwa na kiwango chetu cha kutisha. Kuna mambo ambayo mnaweza kuyaona nje, lakini yale yaliyofichika nyuma ya pazia sisi viongozi tunayafahamu na tulikuwa tukishughulika nayo,” alisema Kamwe.

Hata hivyo, Kamwe alisisitiza kuwa ushindi huo ulikuwa wa thamani kubwa katika kuendeleza mbio zao za ubingwa msimu huu, huku akionyesha kufurahishwa na kurejea kwa mshambuliaji Clement Mzize aliyefunga bao pekee la ushindi.

“Kwa leo, Alhamdulillah, tumepata ushindi muhimu kweli kweli. Bao limefungwa na mchezaji muhimu ambaye naamini atakuwa sehemu ya kutuletea furaha msimu huu, Inshaallah,” aliongeza Kamwe.

Kauli hii ya Kamwe inaashiria kuwa benchi la ufundi na uongozi wa Yanga una kazi ya ziada kurejesha utulivu na kiwango bora cha timu hiyo, huku kurejea kwa Mzize kukiongeza hamasa na matumaini mapya katika safu ya ushambuliaji kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu.

Honour Janza Kateuliwa Kuwa Mkurugenzi wa Ufundi Simba SC Ali Kamwe Aipa Onyo Zito Simba SC: “Pointi 5 Ni Kama Mbili, Wafunge Mikanda!”