Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA KUTOKUWA NA FURAHA KUTAKA ‘KUSEPA’ SIMBA….ONYANGO AVUNJA UKIMYA….AIBUKA NA KUTOA KAULI YAKE RASMI…

admin August 26, 2022 10:05 am


Ujio wa beki wa kati kutoka Burkina Faso, Mohamed Ouattara ndani ya Simba umemfanya Mkenya Joash Onyango kupigwa benchi na Kocha Zoran Maki kiasi cha kukosa mechi mbili za awali za Ligi Kuu Bara sambamba na ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Kumbe kitendo hicho cha kukalishwa benchi, kinamuuma Mkenya huyo na sasa amepanga kutuma maombi ya kutaka kuvunjwa mkataba ili asepe zake sehemu ambayo itamfanya acheze kama ilivyokuwa kabla ya ujio wa Kocha Maki na Ouattara.

Ouattara ambaye amesajiliwa kwa mapendekezo ya Zoran aliyefanya naye kazi katika klabu kadhaa ikiwamo Al Hilal ya Sudan na Wydad Casablanca ya Morocco ameingia kikosi cha kwanza akitengeneza pacha na Henock Inonga na kumng’oa Onyangoi.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Mkenya huyo zinasema huenda akapeleka maombi ya kuvunjiwa mkataba kutokana na kukosa furaha na kushindwa kupewa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Onyango alipotafutwa ili kuthibitisha taarifa hizo alisema:

“Kazi yangu ni kucheza mpira haya masuala ya kimkataba nadhani yanakuwa na usiri mkubwa ndani yake ila kama kuna lolote ngoja tuone.”

WAKIJUA WATACHEZA NA SIMBA HIVI KARIBUNI…KMC WAANZA  MBWEMWE HIZI ZA HATARI…WAPANGA KUJA KWA STAILI MPYA… RASMI….ISHU YA KAPAMA NA AKPAN KUSEPA SIMBA YAFUNGWA ….KOCHA MAKI ATOA TAMKO JINGINE..MABOSI SIMBA WASHINDWA ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply