Habari za michezo

RASMI…UJIO WA KISINDA WAMUWEKA KANDO KAMBOLE…YACOUBA, MAKAMBO NA MOLOKO KUCHUNGUZWA…

admin September 4, 2022 12:51 pm


YANGA imetengeneza mfumo mpya chini ya Rais wake, Mhandisi Hersi Said ambapo mastaa wao wanaopata shida wanawasaidia kila kitu, huku wakiwalipa mishahara na haki zao zingine ikiwamo bima za afya na posho.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, licha ya kumuengua Yacouba katika orodha ya mastaa wao msimu huu, bado wapo naye kikosini ambapo anafanya mazoezi na akiendelea kuonyesha kiwango bora kumshawishi kocha Nabi.

Ukiachana na Yacouba ambaye sifa yake ni kasi, lakini Mzambia Lazarous Kambole aliyesajiliwa hivi karibuni ameondolewa kwenye usajili kumpisha Tuisila Kisinda anayetarajiwa kutua muda wowote na klabu itaendelea kuwa nae na kumlipa stahiki zote lakini hatatumika kwani Yanga tayari ina wachezaji 12 wa kigeni.

Kambole ambaye amesajiliwa kutoka Kaizer Chiefs hajapata nafasi ya kuitumikia timu hiyo kwenye mechi za mashindano kutokana na kupata majeraha kwenye mechi ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Namungo mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Avic Town Kigamboni.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwenye uongozi kilisema kwamba wachezaji hao ni muhimu kwa Yanga na wanafikiria lolote linaweza kutokea kabla ya usajili wa Krisimasi. Wachezaji walioko kwenye hatari ya kuwapisha Kambole na Yacouba kwenye dirisha hilo ni Lucapel Moloko na Makambo ambao wanamulikwa kwa karibu sana na Nabi.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Saad Kawemba, alisema ni lazima sheria ifuatwe hivyo wachezaji waliowasajili ni mali ya Yanga lakini kati yao hao 14 wawili watabaki kuwa mali ya timu na 12 wamesajiliwa.

β€œWote waliopo ni mali ya klabu wataendelea kuwepo watahudumiwa na klabu na wataendelea kuwepo kikosini,”alisema Kawemba ambae aliwahi kuwa kiongozi wa TFF, Mtibwa na Azam kwa nyakati tofauti.

PAMOJA NA TRY AGAIN KUINGILIA KATI…ONYANGO NA SIMBA BADO MAMBO MAGUMU AISEE….ATAKA KUVUNJA MKATABA… BAADA YA KUSOTEA BENCHI SANA…YANGA WAAMUA KUACHANA NA ‘NINJA’ KWA STAILI HII MPYA…AKIZINGUA NDIO BASI TENA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply