Habari za michezo

BAADA YA COASTA UNION KUTOA TAARIFA YAO JANA…MGUNDA KAONA ISIWE TABU…AAMUA KUJIKABIDHISHA SIMBA MAZIMA…

admin September 9, 2022 10:53 am


Kocha Mkuu wa muda wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema yeye ni Kocha Mkuu wa muda wa Simba hivyo taarifa za Klabu ya Coastal Union hana taarifa nazo.

Mgunda amesema hayo jana Alhamisi, Septemba 8, 2022 akiwa nchini Malawi na Wanamsimbazi kwa ajili ya mechi ya kombe la mabingwa Barani Afrika, ambapo miamba hao wa soka nchini watakipiga kesho Septemba 10 na Nyasa Big Bullets.

“Ukweli ni kwamba mimi sasa ndio Kocha Mkuu wa muda wa Simba wala siyo Costal Union, na nipo huku Malawi kwa asilimia 100% kwa ajili ya kufanya kazi yangu ambayo Simba SC wameona na mimi naweza kutoa mchango wangu.

“Nipo Simba mpaka pale itakapotoka taarifa nyingine, hizo taarifa nyingine zinazosambaa hazina ukweli wowote.

“Kilichonivutia na kunifariji ni namna ambavyo wachezaji walivyokuwa tayari kwenye mazoezi na kutambua uzito wa mechi ya keshokutwa dhidi ya wapinzani wetu,” amesema Mgunda.

SAKATA LA MGUNDA KUKOSA LESENI A YA CAF….TFF WAFUNGA MJADALA RASMI…WATOA ORODHA YA MAKOCHA WENYE LESENI A … UWANJA WA MAJALIWA SASA RASMI KWA MATUMIZI….NAMUNGO FC MENO NNJE…LUSAJO ATIA NENO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply