CAF

FT:…SIMBA NA YANGA ZAFANYA KWELI CAF…PHIRI ARUDIA GOLI LA SAKHO….MAYELE ATEMBEA NA MPIRA JUMLA JUMLA…

admin September 10, 2022 3:42 pm


SIMBA SC wameng’ara  ugenini baada ya kuwachapa wenyeji Big Bullets bao 2-0 mchezo wa  mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika inayopigwa kwenye uwanja wa Taifa Bingu, Malawi.

Moses Phiri aliiandika bao la kwanza Simba mnamo dakika ya 29 na mnamo dakika ya 83 John Bocco aliiandikia timu yake bao la pili.

Timu hizo zitarudiana Septemba 17,mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Aidha katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam, TIMU ya Yanga SC imeanza vyema katika kampeni za kuwania kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa mabao 4-0 wenyeji Zalan FC kutoka nchini Sudan Kusini mchezo wa  mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walipata mabao ya yote manne kipindi cha pili mara baada ya kipindi cha kwanza timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele amefunga hat-trick akifunga dakika 45,85 na 88 huku bao moja likifungwa na Fei Toto dakika ya 55

Yanga watarudiana na Zalan FC Septemba 16,2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa kama wenyeji 

KUELEKEA MECHI NA WASUDAN LEO…MORRISON SURE BOY WAWEKWA NNJE YANGA…KAZE AFUNGUKA A-Z ISHU ILIVYOKUWA… MZIMU WA MOSIMANE WAENDELEA KUISUMBUA AL AHLY…WAINGIA GHARAMA KUBWA KUMPA KAZI “M’BAYA WA CHELSEA”…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply