Habari za michezo

KISA MAFANIKIO YA SIMBA CAF….MTANGAZAJI AZAM TV ALAZIMIKA KUIOMBA MSAMAHA YANGA…

admin September 11, 2022 12:04 pm


Mtangazaji wa Azam TV, Timzo Karugira amewaomba radhi viongozi, wachezaji, mashabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira nchini kutokana na matamshi yake ya jana kuwa Yanga wameingia katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa mgongo wa Simba Sc, kauli ambayo imeibua mjadala mzito.

Akitangaza jana kabla ya mchezo wa Yanga na Zalan FC ya Sudan Kusini kuanza, Timzo alisema Yanga wameingia katika mashindano ya CAF baada ya kubebwa na watani zao Simba ambao walifanya vizuri katika mashindano hayo msimu uliopita na kusababisha Tanzania kupewa nafasi ya timu nne kushiriki mashindano ya Kimataifa ikiwemo Yanga.

Leo Jumapili, akifuta kauli hiyo, Timzo Karugira amesema Yanga wameingia CAF Champion League kama bingwa wa nchi msimu uliopita (2021/22) tena wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja na siyo kwa mgongo wa watani zao Simba kama alivyosema jana, hivyo alikosea na ameomba Yanga wamsamehe.

KISA KUKOSEKANA KWA DIARA YANGA…MSHERY AWEKA REKODI HII YA KIBABBE CAF…MAMBO YAANZA KUWA MAZURI KWAKE… SHERIA MPYA ZAMKIMBIZA MWINYI ZAHERA DR CONGO….ADAI FAMILIA YAKE INAWASIWASI NA USALAMA WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply