Habari za michezo

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA WAMALAWI….TSHABALALA AFUNGUKA MASTAA WA SIMBA KUINGIA KWA STAILI MPYA…

admin September 18, 2022 7:36 am


Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Mohamed Hussein amesema kuwa Simba SC ni timu kubwa ya mataji hivyo wataenda kupambana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Nyasa Big Bullet.

Mchezo huo utapigwa leo jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar huku Simba SC wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyopata kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini.

Mohamed Hussein alisema kuwa “Kikubwa ni kuendelea kupambana ili tupate matokeo na kuingia kwenye hatua inayofuata, taratibu tutakuwa tunaelekea kwenye malengo yetu.

“Natoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki na tunaahidi kufanya vizuri na kupambana kwa ajili ya viongozi, mashabiki na sisi wenyewe kwani mpira ndio maisha yetu.

“Kikubwa tunachozungumza tukiwa kambini ni kutengeneza kitu kimoja, utamaduni wa klabu na malengo ya klabu kwa msimu husika, Simba ni timu ya mataji lakini pia timu ya mafanikio.”

RASMI…SIMBA WATANGAZA SIKU YA KUACHANA NA MGUNDA…ISHU YA KOCHA MPYA YAWEKWA WAZI… MAAJABU YA AFRIKA….STAA WA SOKA SIERRA LEONE AKATAA KUUZWA TIMU YA ULAYA…MSHIKIA PANGA WAKALA WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply