Habari za michezo
FT: SIMBA 1-0 De AGOSTO….PHIRI AFANYA YALIYOMLETA TZ….MGUNDA AITISHIA CAF…
admin
October 16, 2022
4:43 pm
KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa timu ya Primeiro de Agosto ya nchini Angola 1-0 na kuwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi ya kwanza Simba Sc kushinda 3-1 ugenini.
Mechi hiyo ambayo imepigwa katika dimba la Benjamini Mkapa, Simba Sc imefanikiwa kutawala mchezo na kuwafanya mashabiki ambao waliujaza uwanja kufurahia kandanda safi kutoka kwa mastaa wa timu hiyo.
Ni Moses Phiri ambaye amekuwa moto katika mechi za hivvi karibu amepachika bao safi ambalo liliwafanya Simba Sc kuwahakikishia kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika
Kwa ushindi huo wa Simba, ni sawa na kusema kuwa kocha mkuu Juma Mgunda anaifukuzia rekodi ya kocha bora wa CAF msimu huu endapo ataiwezesha timu yake kufika nusu fainali.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.