Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA JANA…MAYELE AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA KILICHOWAFELISHA…

admin October 17, 2022 4:27 pm

Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele amesema walikua na kila sababu ya kutinga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, endapo wangepata ushindi mzuri Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Jumapili (Oktoba 08).

Katika mchezo huo, Young Africans ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Al Hilal, hali ambayo iliifanya klabu hiyo kuwa na wakati mgumu jana Jumapili (Oktoba 16) ilipocheza ugenini Khartoum-Sudan kwa kuambulia kichapo cha 1-0.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mayele amesema ilitakiwa washinde mchezo wa nyumbani, ili kuufanya mchezo wa ugenini kuwa rahisi.

“Tulikosea sana kutoka sare hapa nyumbani, naamini hilo ndio lilituweka katika mazingira magumu tulipocheza ugenini dhidi ya Al Hilal, kama mambo yangekua mazuri hapa tungefanikiwa kuendelea na Michuano hii.” amesema Meyele

Young Africans imetolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, na jana ilifungwa 1-0 ugenini.

KUHUSU YALE MADAI YA AZAM KUWAWEKEA MADAWA WAARABU…UKWELI WOTE HUU HAPA…WALIANZIA UWANJA WA NDEGE… MO DEWJI ARUDISHA MAJESHI RASMI SIMBA….ATANGAZA KUFANYA MAKUBWA DIRISHA DOGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply