Habari za Yanga leo
Michezo

HAKUNA KULAZA DAMU….BAADA YA KUPASUKA JANA….YANGA WARUDI TZ NA HASIRA….SIMBA WANACHEEKAA…

admin October 17, 2022 10:44 am

Kikosi cha Young Africans kimeanza safari mapema leo Jumatatu, Oktoba 17, 2022 asubuhi kurudi nyumbani ikitokea Sudan kupitia Ethiopia.

Yanga ilikuwa Sudan kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Al Hilal Omdurman katika mechi iliyochezwa Khartoum.

Kwa matokeo hayo, Yanga, ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara wametolewa katika mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa matokeo ya jumla (aggregate 2-1).

Hii ni kufuatia matokeo ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Goli pekee lililofungwa na Mohamed Abdelrahman katika dakika ya tatu ndio limewafungasha virago wawakilishi hao.

Hata hivyo, kuondoshwa kwa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kunaifanya rasmi timu hiyo kuanguka katika kombe la Shirikisho ambapo sasa itacheza na timu moja kwenye hatua ya mchujo ili kusaka nafasi ya kutinga makundi.

KUELEKEA MAKUNDI CAF…SIMBA NA WABABE WA YANGA WAWEKWA KAPU MOJA….ISHU ITAKUWA HIVI… KISA USHINDI WA SIMBA JANA…RAIS SAMIA ATUMA KONGOLE MSIMBAZI…YANGA WACHUNIWA…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply