Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUTUPWA NNJE LIGI YA MABINGWA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…ABADILI GIA ANGANI ‘CHAP’ HARAKA…

admin October 18, 2022 1:17 pm

Ofisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewatuliza wachezaji wa Yanga baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kipigo cha bao 1-0 na AL Hilal juzi Jumapili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; “Football haipo vile tunavyodhani Sisi huku mtaani, wala sio mchezo wenye guarantee ya matokeo utakayo wewe.

Watu wa kisasa wanasema ni mchezo katili, ila tuongezee na bahati, tusipoipata hii na kukubali pia kuna Mipango ya Mungu, tutakuwa hatuitendei haki football yetu.

Rudini mjipange na linalokuja Wachezaji wetu, msihisi Dunia imewaangukia nyie, mna nafasi ya kurejesha heshma yenu wiki ijayo na kurejesha furaha yetu, Uwezo huo mnao, ni fursa adhimu ya kuthibitisha mliteleza na hamkuanguka.

Nawasihi sana sahauni ya Sudan, rejesheni ari na nguvu Jumapili ijayo kisha msubirie kombe la Shirikisho. Bado tuna Imani na nyie na tunajua mtatufurahisha next weekend Insha’Allah.”

KISA KUFUZU MAKUNDI LIGI MABINGWA….KIGOGO SIMBA AFUNGUKA ‘WANAVYOCHEKEA KOONI’…ATAJA MIPANGO… KUELEKEA MECHI NA DABI KESHO KUTWA..AHMED ALLY AIBUKA NA ‘HOJA YA HAJA’ HII KWA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply