Habari za michezo

TAKWIMU ZINAONGEA…HIVI NDIVYO MANULA ANAVYOMTIMULIA DIARRA VUMBI KWA UBORA…

admin October 23, 2022 2:35 pm

Mdaka mishale wa Yanga, Djigui Diarra, kwenye anga la kimataifa amekimbizwa na Aishi Manula maarufu Air Manula wa Simba.

Katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo Yanga na Simba zimecheza msimu huu, Diarra katunguliwa mabao mawili, huku akiwa na clean sheet mbili.

Alifungwa bao mojamoja dhidi ya Al Hilal nyumbani na ugenini kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Manula akifungwa bao moja dhidi ya Primeiro de Agosto ugenini wakati Simba ikishinda 1-3.

Wote wawili wametoka kukamilisha majukumu ya kimataifa ambapo Yanga imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano, huku Simba ikitinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leo Jumapili, makipa hao wanatarajiwa kuwa na kazi ya kuonesha pale Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa Kariakoo Dabi kunako Ligi Kuu Bara.

Manula alikosekana katika mchezo wa Ngao ya Jamii wakati Simba ikifungwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, langoni alikaa Beno Kakolanya.

BOFYA MARA MOJA TU, UIBUKE MSHINDI WA SIMU KALII YA MERIDIANBET… FT: YANGA 1-1 SIMBA….AZIZ KI AKIMBIA NA FUKO LA MAMILIONI YA KINA OKRAH…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply