Habari za michezo

BAADA YA ‘KUMTESA’ MANULA JUZI…AZIZ KI AIBUKA NA HILI JIPYA…AFUNGUKA KUHUSU MAHABA YAKE…

admin October 26, 2022 3:35 pm

AZIZ Ki kiungo mshamuiaji wa Yanga amesema kuwa anapenda kufunga ama kutengeneza nafasi za mabao akiwa ndani ya uwanja.

Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alijiunga na kikosi hicho akitokea ASEC Mimosas.

Oktoba 23,2022 alifunga bao la pili ndani ya ligi ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Nyota huyo amesema:”Ninapenda kufunga na kutengeneza nafasi za mabao nina amini kwamba mashabiki wanapenda kuona haya yanatokea.

“Kikubwa ni ushirikiano na kila mmoja anafanya kazi yake kutimiza majukumu yake hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” .

Leo Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

MZAMIRU AANIKA SIRI ZAKE SIMBA…AFUNGUKA ISHU YA MKUDE KUPIGWA BENCHI HUKU YEYE AKIANZA… PAMOJA NA ‘KUSHAINI’…PHIRI AFUNGUKA MTU ANAYETAKA KUCHEZA NAYE PAMOJA SIMBA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply