Kocha Msaidizi Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU UBORA WA AZAM…MGUNDA KAKUNA KICHWA WEE..KISHA KWA UPOOLE AKASEMA HILI…

admin October 26, 2022 8:58 pm

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema wanakwenda kucheza mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Azam huku wakiwaheshimu klabu hiyo, Lakini watahitaji alama tatu katika mchezo huo.

Mgunda amezungumza kua mchezo wa derby ulishamalizika hivo mchezo unaofuata ni dhidi ya Azam, Na walijua baada ya kumaliza mchezo wa derby mchezo ambao ungefata ni dhidi ya wanalambalamba na kuhusu hilo wameshajiandaa.

Kocha huyo ambaye ameiongoza timu katika mechi 9 huku 7 zikiwa za kimashindano na hajapoteza mchezo hata mmoja, hivo kuelekea mchezo wa Azam watu wana hamu ya kuona kocha kama ataendeleza rekodi yake kutopoteza mchezo mbele ya matajiri hao wa Dar-es-salaam.

Pia Mgunda ameeleza wachezaji ambao watakosekana katika mchezo huo wa kesho ni Israel Mwenda aliepata majeraha atakaa nje kwa wiki mbili, Kanoute ambae anaendelea kuugua, pamoja na Mzamiru Yassin ambae ataukosa mchezo kutokana na kanuni baada ya kupata kadi tatu za njano.

KUELEKEA MECHI YA KESHO …MASTAA HAWA WANNE WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC… M-BET WAFANYA KWELI KWA SIMBA QUEEN’S…WATOA MKATABA MNONO KUPITA YOTE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply