Habari za Azam FC
Azam FC

MAKOCHA ZAIDI YA 100 WAITAKA AZAM FC…..ISHU YA NABI KUTUA CHAMAZI YAIBUKA UPYA…

admin October 28, 2022 5:39 am

Baada ya kutimuliwa kwa kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, Denis Lavagne, Uongozi wa klabu hiyo umepokea zaidi ya maombi 100 ya makocha wanaotaka nafasi hiyo.

Lavagne raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na kikosi cha Azam hivi karibuni alisimamia timu hiyo katika michezo sita na kufanikiwa kushinda mechi tatu na kupoteza tatu.

Akizungumzia mchakato wa kumpata kocha Mkuu, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema tayari wameanza kupokea maombi ya makocha mbalimbali wakihitaji kukinoa kikosi chao.

โ€œTunamshukuru Mungu kikosi kipo salama chini ya Kaimu kocha Mkuu, Kali Ongala.

โ€œTumepokea CV za makocha mbalimbali ambao ni zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya Tanzania wakihitaji kufanya kazi ya kukinoa kikosi chetu.

โ€œUongozi unaendelea kuyafanyia kazi na mchakato ukikamilika basi kocha atatangazwa. Hakuna asiyetamani kufanya kazi na kocha kariba ya Nabi lakini tunamheshimu kwani yupo kwenye timu nyingine.โ€

NABI AFUNGUKA ISHU YA ‘KUMSUSA’ MAYELE JUZI…SABABU NYUMA YA PAZIA NI HIZI HAPA.. PAMOJA NA KUIKOA YANGA JUZI….FEI TOTO AFUNGUKA A-Z ALIYOYAPITIA KABLA YA MECHI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply