Habari za michezo

BECKHAM NA INTER YAKE WAMKOMALIA MESSI…WATAKA JAMBO LIWE HARAKA…

admin November 2, 2022 7:37 pm

Inter Miami imeongeza nguvu ya kutaka kumsajili Lionel Messi baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia.

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentine mwenye miaka 35, anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain.

Wakati miamba hiyo ya Ligue 1 ikitaka kumbakiza, gazeti la The Athletic kwa mshangao liliandika jana kuwa klabu inayomilikiwa na David Beckham ya Ligi ya Marekani, MLS inataka kupambana kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa zamani wa Barcelona.

Mazungumzo yamepangwa kuanza tena baada ya Messi kutoka Qatar, huku Inter Miami ikiwa katika nafasi nzuri ya kumnasa mbele ya mkataba mpya wa kubaki PSG au kurudi Barcelona.

Ndugu wawili, Jorge na Jose Mas ambao pia wanaimiliki Inter pamoja na Beckham wanaongoza mazungumzo hayo.

KARIA : MTANIKUMBUKA…SITAKUFA NITABAKI NIKIWATAZAMA… SIMBA YAANZA KUZITAFUTA 5-0 ZINGINE KWA AJILI YA  SINGIDA BIG STARS…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply