Habari za Yanga
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA YANGA KUWAHI KWENDA TUNISIA MAPEMA….UKWELI WA JAMBO UKO HIVI…

admin November 5, 2022 5:35 am

MAPEMA jana jioni kikosi cha Yanga kimeanza safari kuelekea nchini Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuwakabili wapinzani wao Club Africain.

Jesus Moloko nyota wa Yanga ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye msafara ulioanza safari jana Novemba 4,2022 kuelekea nchini Tunisia.

Bernard Morrison, Khalid Aucho, Fiston Mayele, Diara, Mshery, Kibwana Shomari na Dickson Job nao wapo kwenye msafara huo pia.

Yanga ina kibarua cha kwenda kusaka ushindi kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho nchini Tunisia ukiwa ni mchezo wa pili.

Ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-0 Club Africain hivyo kibarua kwa Yanga ni kusaka ushindi wa aina yoyote ama sare ya kufungana.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo jambo ambalo limewafanya wawahi kuelekea ugenini kufanya maandaalizi ya mwisho.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini wachezaji wapo tayari na ndio maana tumewahi ili kufanya maandalizi muhimu kuelekea kwenye mchezo wetu,” amesema.

MCHAWI YANGA HUYU HAWA…STRAIKA SIMBA AICHAMBUA A-Z…NABI NA KAZE MTEGONI… ODDS BOMBA ZA MERIDIANBET WIKIENDI HII ZIKO HIVI….BET KIDOGO PATA SANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply