Habari za michezo

IMEFICHUKAA…HII HAPA SABABU YA AZIZ KI KUTOKURUDI NA TIMU YANGA…CHANZO NI…

admin November 12, 2022 1:56 pm

MFUNGAJI wa bao lililowavusha Yanga kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Stephen Aziz Ki hajarudi na wenzake kwa ruhusa maalum ya uongozi.

Nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda kwao Bukina Faso baada ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi.

Yanga walitua mchana jana kutoka Tunisia kupitia Dubai na wanatarajia kwenda Mwanza leo saa moja usiku tayari kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wote wamerudi isipokuwa Aziz Ki ambaye hadi kocha Nabi anamalizia msafara wao hakuonekana na kuibua shangwe za mashabiki wakihoji mchezaji huyo yupo wapi?

Aziz Ki amefungiwa mechi tatu na faini laki tano kwa kosa kutosalimiana na wachezaji wenzake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Hivyo staa huyo hatakuwa miongoni mwa wachezaji na benchi la ufundi wanaoanza safari usiku wa leo kwaajili ya mchezo wa ligi huko Mwanza.

USHINDI ZIDI YA WAARABU WAIONGEZA YANGA JEURI…WATANGAZA KUSEPA NA KILA KITU… KUMEKUCHA SIMBA…ACHANA NA MANZOKI…STRAIKA HILI LA MABAO LANUKIA MSIMBAZI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply