Habari za Michezo leo
Habari za michezo

INJINIA HERSI USO KWA USO NA MANGUNGU….WADAU WAPISHA WAKAE WENYEWE…

admin November 14, 2022 3:29 pm

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said na Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu ni miongoni mwa watu ambao wamehudhuria mkutano mkuu wa 17 wa Kawiada wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaofanyika leo Novemba 14 jijini Mwanza.

Viongozi hao wamekaa meza moja wakifuatana, ambapo Mangungu alifika mapema na kukaribishwa kwenye meza hiyo ambayo pia wamekaa viongozi wa KMC na Azam huku Hersi akifika baadaye na kukaribishwa kukaa kwenye meza hiyo katika kiti cha karibu na Mangungu.

Baada ya Hersi kufika alikaribishwa na viongozi wenzake wa klabu za Ligi Kuu waliokaa kwenye meza hiyo kisha akawasalimia na kushikana mkono na Mangungu na kuketi kwenye kiti.

Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF, wafanyakazi wa TFF, viongozi wa Kanda za michezo nchini, viongozi wa klabu za Ligi Kuu na wageni waalikwa.

Baadhi ya viongozi wengine ambao wamehudhuria mkutano huo ni pamoja na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Steven Mashishanga na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Mecky Sadick.

Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza kujadili ajenda mbalimbali.

HUYU NI MFALME WA MERIDIAN USSD BETI NA KITOCHI…ASHINDA MAMILIONI KIRAHISII… EHEE…MASTAA BONGO WAMVULIA KOFIA ‘BABU KAJU’…KAPOMBE KASHINDWA KUJIZUIA KAFUNGUKA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply