Habari za michezo

SIMBA WAMRUKA FUTI MIA MWARAMI….WAMKANA KAMA YUDA ALIVYOMKANA YESU….

admin November 15, 2022 10:17 pm

Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekua Kocha wa magoli kipa Muharami Said Mohammed maarufu Shilton hakua muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakua na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.

HUYU HAPA MTZ ALIYETOBOA BILA SIMBA NA YANGA …KUTOKA KUCHEZA CHANDIMU MPAKA KUSAJILIWA NNJE YA NCHI.. CAF YAZIPA SIMBA NA YANGA WAARABU….MASHINE HIZI SABA KUTEMWA MSIMBAZI….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply